23 Juni 2020 - 11:38
Al Hashd al Shaabi: Oparesheni ya jeshi la Iraq itaendelea hadi kuangamizwa Daesh

Kamanda wa oparesheni ya kikosi cha harakati ya al Hashd al Shaabi katika mkoa wa Diyala nchini Iraq amesema kuwa awamu ya tatu ya "Oparesheni ya Ushindi wa Mashujaa wa Iraq" itaendelea mashariki na kaskazini mwa nchi hadi mabaki yote ya kundi la kigaidi la Daesh yatakapoangamizwa kikamilifu.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Talib al Mousawi amesema kuwa kikosi cha wapiganaji wa al Hashd al Shaabi asubuhi ya jana Jumatatu kilianzisha awamu ya tatu ya mashambulizi yaliyopewa jina la Operesheni ya Mshujaa wa Iraq kikisaidiwa na ndege za kivita za jeshi la taifa kwa ajili ya kuliangamiza kikamilifu kundi la Daesh na kudhamini usalama wa maeneo ya mashariki mwa mkoa wa Salahuddin, magharibi mwa mkoa Diyala na kusini magharibi mwa Kirkuk. 

Kamanda wa kikosi cha al Hashd al Shaabi katika mkoa wa Diyala ameongeza kuwa oparesheni hiyo inatekelezwa kwa kuvishirikisha vikosi saba vya kujitolea vya wananchi, kikosi cha makomando, kikosi cha anga, jeshi na polisi ya Iraq.  

Katika miezi ya karibuni, mashambulizi ya kundi la kigaidi la Daesh yameongezeka hususan katika maeneo kati ya mikoa ya Kirkuk, Salahuddin na Diyala maarufu kwa  jina la " Pembe Tatu za Mauti".


342/